BERLIN: Maafikiano kukusanya data kupiga vita ugaidi
5 Septemba 2006Waziri wa ndani wa Ujerumani na mawaziri wenzake wa majimbo wamekubaliana na mpango wa hatua za kuchukuliwa kupambana na ugaidi.Miongoni mwa hatua zilizokubaliwa katika mkutano wa mawaziri hao wa ndani,mjini Berlin,ni kufungua kituo kipya kitakachokusanya habari kwa azma ya kuwasaidia wachunguzi kuwasaka wale wanaoshukiwa kuhusika na ugaidi.Baadhi ya mawaziri wa mrengo wa kushoto wana khofu kuwa kituo hicho cha kukusanya habari za raia kitazidi kuondoa uhuru wa kimsingi.Kwa upande mwingine mawaziri wa kihafidhina wametaka kituo hicho kikusanye pia habari zinazohusika na dini,uwepo ukaguzi zaidi kwa njia ya kamera za video na wageni wanaoshukiwa kuwa magaidi wachunguzwe kwa vibandiko vya elektroni.Hatua za kuimarisha njia za kupambana na ugaidi zinafuatia jeribio liloshindwa kufanikiwa kuripua mabomu katika treni mbili za abiria nchini Ujerumani, mwisho wa mwezi Julai.