BERLIN : Monyesho ya Ukuta wa Berlin yafungwa
9 Aprili 2005Matangazo
Maonyesho tata ya nje mjini Berlin kwa ajili ya kumbukumbu ya mamia ya watu waliouwawa wakijaribu kuitoroka Ujerumani ya Mashariki yamemuariwa kufungwa na mahkama ya mkoa.
Mahakimu wamehukumu kwamba mamia ya misalaba ya mbao na sehemu iliojengwa upya ya Ukuta wa Berlin lazima viondolewe kwa sababu mkataba wa kukodisha ardhi hiyo sio halali tena.Wanasiasa kutoka chama tawala cha SPD mjini Berlin na chama cha kikomunisti cha zamani cha PDS wamekuwa wakishutumu maonyesho ya misalaba hiyo kuwa sio ya ustaarabu.
Vvyombo vya habari vya ndani ya nchi pia vimekuwa vikishutumu maonyesho hayo ambapo watalii wamekuwa wakipiga picha na kuweza kununuwa kumbukumbu halisi za mabaki ya Vita Baridi.