BERLIN : Mwenyekiti wa bodi ya Siemens kujiuzulu
20 Aprili 2007Vyombo vya habari nchini Ujerumani vinaripoti kwamba mwenyekiti wa bodi ya Siemens kampuni kubwa kabisa ya Kijerumani Heinrich von Pierer atatangaza kujiuzulu kwake leo hii.
Gazeti mashuhuri la Bild limesema von Pierer ataachia wadhifa wake katika mkutano ujao wa bodi hapo tarehe 25 mwezi wa April.Von Pierer amesema anajiuzulu ili kuwajibika binafsi kwa uchunguzi wa rushwa wa kampuni hiyo yenye makao yake mjini Munich.
Waendesha mashtaka wanachunguza madai ya malipo yasio halali ya kujipatia biashara nchi za nje na wakuu watendaji wa hivi sasa na wa zamani wamehojiwa.
Kwa mujibu wa taarifa ya kampuni hiyo mwanachama wa bodi Gerhard Cromme atachukuwa nafasi ya von Pierer ambaye kipindi chake cha uongozi kilikuwa kimalizike mwakani.