1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Mwito kwa Burma kumuachilia huru Suu Kyi

18 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF2V

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani,Joschka Fischer,ametoa mwito kwa serikali ya Burma kuwaachilia huru wafungwa wote wa kisiasa.Katika risala iliyoelekezwa kwa kiongozi wa upinzani nchini Burma,Aung San Suu Kyi,waziri Fischer amesema serikali ya Ujerumani na Umoja wa Ulaya pia unaishinikiza serikali ya Burma ifanye majadiliano pamoja na makundi ya kidemokrasia nchini humo.Hapo awali Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan,waziri wa kigeni wa Marekani, Condoleezza Rice na Halmashauri ya zawadi ya Nobel nchini Norway walitoa mwito wa kumuachilia huru Suu Kyi ambae yupo kwenye kifungo cha kubakia nyumbani kwake.Aung San Suu Kyi alietunzwa zawadi ya amani ya Nobel anatimiza umri wa miaka 60 siku ya jumapili.