1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Siemens yathibitisha kuwa inachunguzwa.

26 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC6s

Kampuni kubwa la uhandisi nchini Ujerumani Siemens limethibitisha kuwa linachunguzwa na chombo cha soko la hisa la Marekani kwa madai ya rushwa.

Tume ya soko la hisa la Marekani itafanya uchunguzi wake rasmi juu ya madai hayo kuwa Siemens ilitenga fedha za hongo zilipatazo Euro milioni 400.

Afisa mtendaji mkuu wa Siemens Klaus Kleinfeld ametangaza jana kuwa ataondoka madarakani ifikapo Septemba ili kuruhusu Siemens kuangalia iwapo wanaweza kupunguza kasi ya kashfa hiyo.

Kleinfeld , hata hivyo hajahusishwa binafsi na uchunguzi wa kashfa hiyo.

Siemens inaunda matreni, na mitambo ya nishati, na mitambo ya hospitali na mawasiliano. Ni mwajiri mkubwa nchini Ujerumani na zaidi ya watu 450,000 wanafanyakazi katika kampuni hilo duniani kote.