Berlin. Wajerumani washutumu siasa kali za mrengo wa kulia katika maandamano.
12 Novemba 2006Matangazo
Katika mji mkuu wa Ujerumani , Berlin mamia ya watu wamefanya maandamano ya amani kupinga dhidi ya mkutano mjini humo wa chama chenye msimamo mkali wa mrengo wa kulia, cha NPD.
Kiasi watu wanaokadiriwa kufikia 400 waliandamana wakiwazomea wajumbe 500 wa chama cha NPD ambao wamejikusanya kwa ajili ya mkutano wa chama chao.
Chama cha NPD kina viti vichache katika mabaraza mawili ya majimbo katika eneo la mashariki ya Ujerumani lakini hakina viti katika bunge la shirikisho.