Berlin. Waliotekwa nyara Nigeria waachwa huru.
19 Juni 2005Matangazo
Wizara ya mambo ya kigeni ya Ujerumani imetangaza kuwa wafanyakazi wawili wa Kijerumani wa makampuni ya kuchimba mafuta ambao walitekwa nyara kusini mwa Nigeria siku ya Jumatano wameachiliwa huru bila madhara.
Mateka wengine wanne wa Kinigeria, pia nao wameachiwa.
Wafanyakazi hao , ambao wanafanyakazi katika kampuni la Shell , waliachwa huru kufuatia mazungumzo kati ya watekanyara hao na maafisa wa serikali ya jimbo la Bayelsa.
Msemaji wa serikali amesema kuwa watu hao waliachwa huru bila masharti.