1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin yachunguza ripoti za wakosoaji wa Urusi kupewa sumu

22 Mei 2023

Polisi nchini Ujerumani imeanzisha uchunguzi kuhusu uwezekano wa kupewa sumu Warusi wawili wanaoishi uhamishoni.

https://p.dw.com/p/4ReUc
Symbolbild Gift Flasche Alkohol
Picha: Fotolia/pzAxe

Waathiriwa hao walihudhuria mkutano ulioandaliwa na mkosoaji wa Rais wa Urusi Vladmir Putin mjini Berlin mwezi uliopita. Mmoja ni mwandishi habari aliyeondoka Urusi hivi karibuni. Mwandishi huyo alipatwa na dalili zisizojulikana wakati wa mkutano huo lakini akasema dalili hizo huenda zilikuwepo kabla ya mkutano huo.

Mshirika wa pili ni Natalia Arno anayeishi Marekani, ambaye ni mkurugenzi wa Wakfu wa Free Russia nchini Marekani. Arno aliandika kwenye Facebook kuwa alidhani kuwa alikuwa na uchovu kutokana na safari ya ndege wakati alipoanza kujisikia vibaya akiwa Berlin. Kisha alikwenda Prague, ambalo alisema alipata mlango wa chumba chake hotelini ukiwa wazi.

Soma pia:Ujerumani yachunguza madai ya kupewa sumu mwandishi wa habari 

Wakosoaji kadhaa wa Urusi, akiwemo kiongozi wa upinzani Alexy Navalny na mwandishi habari Vladmir Kara-Murza, wanawatuhumu maafisa wa Urusi kwa kuwapa sumu katika siku za nyuma. Moscow inakanusha madai hayo.