1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Katibu Mkuu Annan ataka mikakati endelevu juu ya kuisaidia JK:Kongo

11 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG8j

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa bwana Kofi Annan amezitaka nchi za Umoja wa Ulaya ziwe na mipango ya muda mrefu katika jukumu la kulinda amani nchini Jamhuri ya kidemokrasi ya kongo.

Akizungumza kwenye mhadhara ulioandaliwa na wakfu wa Bartelsmann mjini Berlin,katibu Mkuu Annan amesema anatumai kuwa jukumu la kulinda amani nchini Kongo halitaishia katika kuhakikisha kufanyika uchaguzi huru tu.

Amesema, baada ya uchaguzi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo itahitaji msaada wa kuleta mageuzi katika mfumo wake wa usalama ,mafunzo kwa ajili ya polisi na kuufanya uongozi wa serikali uwe bora zaidi.

Nchi za Umoja wa Ulaya ikiwa pamoja na Ujerumani zimepeleka majeshi ili kulinda amani wakati wa uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo utakaofanyika mwishoni mwa mwezi huu.