1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Mkutano wa CDU/CSU na Kijani wamalizika bila maafikiano

23 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEYI

Madhamana wa vyama vya kihafidhina vya CDU /CSU na chama cha kijani wamemaliza mkutano wao mjini Berlin hii leo bila kufikiwa mapatano. Mwenyekiti wa chama cha CDU Angela Merkel amesema kwa sasa pande hizo mbili hazitokutana tena.

Lengo la mazungumzo hayo yalikuwa ni kupima uwezekano wa kuundwa serikali ya muungano wa vyama vitatu vya wahafidhina,Waliberali wa FDP na walinzi wa Mazingira-Die Gune.

Angela Merkel na kiongozi wa chama ndugu CSU bwana Edmund Stoiber wamethibitisha kwamba kuna tofauti kubwa kati ya vyama vyao na wanamazingira.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha wanamazingira-Die Grüne bwana Reinhard Bütikofer amesema mazungumzo hayo yameonyesha tofauti zilizopo kati ya chama chake na vyama ndugu vya CDU/CSU.

Vyama vya CDU/CSU vitafanya mkutano wa pili siku ya jumatano na chama cha Kansela Gerhard Schöder SPD.