1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin:Onyo la Kofi Annan

12 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFsi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan, leo ameonya kuwa mivutano inazidi kuongezeka kati ya raia wa nchi za Magharibi na Waislamu. Amewaomba watu kuwa na misimamo sawa kati ya tamaduni zao. Bw. Annan, akiwahutubia Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tübingen, kilichoko kusini mwa Ujerumani, amesema kuwa ni sawa kabisa kulaumu mashambulio kama yale yaliyofanywa na al Qaida Septemba 11 mwaka wa juzi nchini Marekani. Lakini watu wanapaswa kuwa waangalifu zaidi ili wasisababishe uhasama kati ya raia wa nchi za Magharibi na Waislamu. Ameongeza kusema kuwa ni makosa makubwa kujifanya kama kwamba uislamu na ustaarabu wa nchi za Magharibi ni vitu vinavyotofautiana. Havitofautiani hata kidogo kwani kuna Waislamu millioni kadhaa wanaoishi nchini Ujerumani na katika nchi nyingine za Magharibi wanaofahamu hivyo. Lakini wengi wa Waislamu hao sasa wanajikuta wakishukiwa, wakiandamwa na kubaguliwa kwa sababu baadhi ya nchi za Kiislamu zinahisi kuwa ye yote yule anayeshirikiana na nchi za Magharibi au anayefuata utamaduni wake atakiona cha mtema kuni au nguvu inatumiwa dhidi yake.