1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

"Biashara badala ya ishara"

Maja Dreyer16 Oktoba 2007

Mada ambayo inazingatiwa hasa leo hii ni mazungumzo kati ya rais Putin wa Urusi na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel. Suali ni je, mkutano huu ulifanikiwa au la?

https://p.dw.com/p/C7lL
Mazugumzo yalikuaje?
Mazugumzo yalikuaje?Picha: picture-alliance/dpa

Tuanze basi na uchambuzi wa gazeti la “Rhein-Zeitung”. Limeandika:

“Hali ya mkutano huu ilikuwa ya kuridhiana. Inaonekana kama Kansela Merkel na Rais Putin walifanikiwa kutafuta namna na kuzungumza ambayo ni juu ya masuala yenyewe na si tu ya kirafiki. La muhimu ni biashara na si ishara. Inaruhusiwa kutaja ukosoaji. Bila shaka, Angela Merkel baada ya kustaafu kisiasa hatapewa mkataba kama mshauri wa kampuni ya kiserikali ya Urusi kama mtangulizi wake Gerhard Schröder ambaye alionyesha urafiki mkubwa na rais Putin. Kwa upande mwingine lakini, Angela Merkel anathubutu kuzungumzia wazi tofauti za maoni na hata pamoja na hayo anaheshimika huko Urusi. Kwa hivyo, uhusiano kati ya Ujerumani na Urusi ni wa kuaminika kuliko zamani katika wakati wa Kansela Schröder.”

Gazeti la “Wiesbadener Kurier” linaangalia ushirikiano katika sekta ya nishati kati ya Ujerumani na Urusi na linachambua kuwa:

“Serikali ya Urusi ilikubali kampuni kubwa ya nishati ya Ujerumani inunue kampuni ya nishati ya Urusi. Hii ni kama ishara kwa Umoja wa Ulaya, kwamba Ulaya itoe ruhusa pia kwa makampuni ya Kirusi kuwekeza katika uchumi ya Ulaya. Kwa maoni ya Putin, Ujerumani inapaswa kuwa mfano katika ushirikano na Urusi katika sekta ya nishati, uhusiano hauna budi uongezwe siku za usoni. Kansela Angela Merkel aliyajibu haya kwa kukubali njia ya bomba la gesi ya ardhi kupitia bahari ya Baltic – licha ya kwamba nchi za Ulaya Mashariki zinapinga mpango huu.”

Ni gazeti la “Wiesbadener Kurier”. Suala lingine muhimu kuhusiana na uhusiano kati ya Urusi na nchi za Magharibi ni lile na usalama ambapo kuna tofauti za misimamo. Zaidi ameandika yafuatayo mhariri wa “Märkische Oderzeitung”:

“Wakati ushirikiano katika uchumi na sayansi unaonekana kama utakuwa wa karibu, mivutano kuhusiana na usalama inakuwa mikali zaidi. Kama jibu juu ya mpango wa Marekani kujenga mitambo ya kufyetua makombora huko Ulaya Mashariki, rais Putin alitishia Urusi itakiuka mkataba juu silaha za kinyuklia. Jibu hilo kali lakini linafahamika. Ukiangalia sera za kimataifa, Urusi iko katika hali ngumu. Shirika la Kujihami la Magharibi NATO limekua lilielekea upande kwa Mashariki na Marekani hata ina vituo vya kijeshi katika nchi ambazo zamani zilikuwa ndani ya Umoja wa Kisoviet. Hata hivyo, uwezekano wa vita vyengine vya baridi si mkubwa, kwa sababu wanasiasa wengi wenye nguvu katika serikali ya Urusi wanapendelea ushirikiano badala ya kuongeza nguvu ya kijeshi.”

Na hatimaye tuelekee China ambapo wiki hii chama tawala cha kikomunisti kinafanya mkutano wake mkuu. Mhariri wa “Magdeburger Volksstimme” anafuatilia siasa za China na ameandika:

“Kulingana na mkuu wa chama ya kikomunisti Hu Jintao, China iko njiani kuimarisha usalama wa jamii yake. Demokrasi haiko katika mbinu hii. Kwa hivyo, China inabakia kwenye kanuni zake, pia juu ya suala la Taiwan. Kisiwa hiki ambacho kinataka kujitegemea hakiwezi kuipinga serikali ya China yenye nguvu zaidi ya kisiasa na kijeshi. Nchi za Magharibi zinakaa kimya kuhusu suala hilo. Lakini kweli ni jambo la kushangaa kwamba Ujerumani au Marekani zinamwalika rasmi Dalai Lama wa Tibet na hivyo kuhatarisha mahusiano yao na China, wakati suala la Taiwan linaachiliwa mbali.”