BIASHARA NA KAZAKHSTAN ITAIMARISHWA:
5 Desemba 2003Matangazo
ASTANA: Kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani amekutana na Rais Nursultan Nazerbayev wa Kazakhstan kwa mazungumzo yenye nia ya kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili.Baada ya mazungumzo yao katika mji mkuu WA Kazakhstan-Astana,Kansela Schroeder amesema biashara itaongezwa kwa mara mbili katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.Kwa hivi sasa thamani ya biashara inayofanywa na Ujerumani pamoja na Kazakhstan ni kiasi cha Euro bilioni 1.8 kila mwaka.