Biden ayatembelea makaburi ya kijeshi ya Marekani Ufaransa
9 Juni 2024Biden anatumai kuwa hatua hiyo ya leo itamuongezea kura katika uchaguzi wa urais wa Marekani mwezi Septemba.
Kabla ya kurejea Marekani, Biden alitoa heshima kwa wanajeshi waliouawa, katika makaburi ya Kimarekani ya Aisne-Marne, yaliyoko nje ya mji mkuu Paris.
Soma pia: Macron kumpokea Biden katika ziara rasmi mjini Paris
Aliweka shada la maua kwenye kanisa la makaburi hayo walikozikwa karibu askari 2,200 wa Kimarekani waliopigana katika Vita Vya Kwanza Vikuu vya Dunia.
Ziara ya Biden nchini Ufaransa iliashiria miaka 80 ya kumbukumbu ya D-Day ambayo ni operesheni ya vikosi vya washirika wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia iliyopelekea kuangushwa kwa utawala wa Kinazi nchini Ujerumani.
Aidha Biden alitumia ziara hiyo kusherehekea ushirikiano kati ya Marekani na Ufaransa.