1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Biden na Scholz kufanya mazungumzo Februari 9, White House

27 Januari 2024

Rais Joe Biden wa Marekani na Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani wanatarajiwa kufanya mazungumzo katika Ikulu ya White House mnamo Februari 9, 2024.

https://p.dw.com/p/4bkYE
Mkutano wa kilele wa G7 Japan, Hiroshima | Joe Biden na Olaf Scholz
Rais wa Marekani Joe Biden akiwa na kansela wa Ujerumani Olaf Scholz katika mkutano wa G7 huko Hiroshima. Viongozi hawa wanatarajia kukutana mwanzoni mwa FebruariPicha: Jonathan Ernst/Pool/REUTERS

Ikulu ya Marekani imesema viongozi hao wawili watasisitiza kwa mara nyingine uungaji wao mkono wa kuilinda ardhi ya Ukraine na watu wake dhidi ya uchokozi wa Urusi.

Hata hivyo Marekani kwa sasa haina fedha kwa ajili ya Ukraine, na imeshindwa kupeleka risasi na makombora ambayo Kyiv inayahitaji ili kupambana na Urusi.

Serikali ya Biden tayari imetumia dola bilioni 111 kwa ajili ya misaada ya kijeshi na kibinadamu tangu Urusi ilipoivamia Ukraine Februari 2022.

Soma pia:Sunak atangaza msaada mpya wa mabilioni ya dola kwa Ukraine

Msaada mpya wa Biden wa dola bilioni 110 kwa Ukraine, Israel na mahitaji mengine ya usalama wa taifa umekwama kutokana na mvutano kati ya bunge na White House juu ya vipaumbele vingine vya kisera, ambavyo ni pamoja na usalama wa ziada kwenye mpaka wa Marekani na Mexico.