1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Biden aonya juu ya tishio kwa demokrasia Marekani

16 Januari 2025

Rais wa Marekani anayeondoka madarakani Joe Biden amesema Marekani inaangukia mikononi mwa matajiri wachache ambao matokeo yake ni hatari ikiwa hawatadhibitiwa.

https://p.dw.com/p/4pCHo
Washington Marekani 2025 | Rais Biden akilihutubia taifa katika ikulu yake
Bila kuwataja moja kwa moja, Biden aliwakusudia mabilionea ambao wameonekana kumuunga mkono TrumpPicha: Mandel Ngan/AFP/Getty Images

Biden ambaye anatarajia kukabidhi madaraka kwa rais mteule Donald Trump Januari 20, amesema katika hotuba yake ya kuaga kuwa utawala wa matajiri hao unachora sura mpya ya Marekani na unatishia demokrasia, haki za msingi pamoja na uhuru.

Bila kuwataja, Biden aliwakusudia mabilionea ambao wameonekana kumuunga mkono Trump ikiwa ni pamoja na Mmiliki wa kampuni ya Tesla Elon Musk, mmiliki wa kampuni ya Amazon Jeff Bezos na Mark Zuckerberg anayemiliki kampuni ya Meta inayojumuisha mitandao ya kijamii ya Facebook na Instagram.

Biden ambaye ni rais wa 46 wa Marekani ametaja kusikitishwa na kitendo cha kusambazwa kwa msururu wa taarifa potofu akitaka mitandao ya kijamii kuwajibishwa na kuwepo sheria ya kudhibiti matumizi ya akili mnemba (AI).