1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden kukutana ana kwa ana na Xi katika mkutano wa APEC

Sylvia Mwehozi
13 Novemba 2023

Rais Joe Biden wa Marekani mnamo wiki anatarajiwa kukutana ana kwa ana na Rais wa China Xi Jinping, ikiwa ni mara ya kwanza ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.

https://p.dw.com/p/4YjAP
Mkutano wa Xi na Biden
Rais wa China Xi Jinping akisalimiana kwa mkono na Rais Joe Biden wa Marekani mwaka 2022.Picha: Kevin Lamarque/REUTERS

Rais Joe Biden wa Marekani mnamo wiki anatarajiwa kukutana ana kwa ana na Rais wa China Xi Jinping, ikiwa ni mara ya kwanza ndani ya kipindi cha mwaka mmoja. Viongozi hao watakutana pembezoni mwa mkutano wa kilele wa Jukwaa la ushirikiano wa kiuchumi wa nchi za kanda ya Asia na Pasifiki APEC, utakaofanyika San Francisco Marekani siku ya Jumatano.

Kwa mujibu wa mshauri wa usalama wa taifa wa Marekani Jake Sullivan, Rais Biden anataka kuanzisha tena uhusiano wa kijeshi na China. Kando na hilo, mazungumzo ya viongozi hao yatatawaliwa na masuala tete ya kimataifa, kuanzia vita vya Israel na Hamas hadi uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine, uhusiano wa kibiashara, miongoni mwa ajenda nyingine.

Kuelekea mkutano huo mamia ya waandamanaji, walikusanyika jana mjini San Francisco kupinga Jukwaa hilo.