Biden kukutana na Netanyahu
25 Julai 2024Matangazo
Mkutano kati ya viongozi hao wawili unafanyika baada ya Netanyahu kutoa hotuba ya mashambulizi mbele ya bunge la Marekani jana Jumatano, ambapo pia aliiomba Marekani na Israel kusimama bega kwa bega kuikabili Iran aliyoitaja kama adui.
Mvutano kati ya viongozi wa mataifa hayo umeongezeka na hasa kutokana na hatua za serikali ya Israel katika Ukanda wa Gaza.
Netanyahu pia anatarajiwa kukutana na mgombea mpya wa Chama cha Democratic, Kamala Harris, baadae leo na kesho Ijumaa atafanya mazungumzo na mgombea wa Republican, Donald Trump kwenye makazi yake huko Mar-a-Lago, Florida.