1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden kuomba fedha bungeni kwa ajili ya Israel na Ukraine

Sylvia Mwehozi
20 Oktoba 2023

Rais wa Marekani Joe Biden amewasilisha mpango wake wa kuomba msaada zaidi wa kifedha bungeni na umma wa Wamarekani ili kuiunga mkono Israel na Ukraine.

https://p.dw.com/p/4XmLH
Washington-Rais Joe Biden
Rais wa Marekani Joe BidenPicha: Jonathan Ernst/AFP

Rais wa Marekani Joe Biden amewasilisha mpango wake wa kuomba msaada zaidi wa kifedha bungeni na umma wa Wamarekani ili kuiunga mkono Israel na Ukraine. Katika hotuba yake ya nadra kwenye ofisi ya Rais, maarufu kama Oval Room, Biden amesema ikiwa alichokiita "uchokozi wa kimataifa" kitaruhusiwa kuendelea, basi kuna hatari ya migogoro na machafuko kuweza kuenea katika sehemu nyingine za ulimwengu. Biden amelifananisha kundi la Hamas na Putin akisema kuwa wanawakilisha vitisho tofauti lakini wanafanana kwa azma ya kuangamiza taifa jirani la kidemokrasia.

Aidha rais huyo amesisitiza kwamba ushindi wa Israel na Ukraine katika vita vyao ni suala lenye umuhimu mkubwa kwa usalama wa Washington. Hii leo, Biden atawasilisha ombi la dola bilioni 100 za ufadhili wa dharura. Sehemu kubwa ya ufadhili huo itaelekezwa katika vita vya Ukraine. Fedha nyingine ni kwa ajili ya Israel pamoja na ulinzi katika eneo la Indo-Pacific.