1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden kuyatembelea maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Helene

Josephat Charo
30 Septemba 2024

Kimbunga Helene kimesababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu ya mifumo ya maji, mawasiliano, barabara, njia muhimu za usafiri, pamoja na makazi kadhaa.

https://p.dw.com/p/4lDUk
Rais Joe Biden wa Marekani
Rais Joe Biden wa MarekaniPicha: ANDREW CABALLERO-REYNOLDS/AFP

Rais wa Marekani Joe Biden anasema atalitelembea eneo lililoathirwa na kimbumga Helene kama hakitatiza operesheni za uokozi na ujenzi mpya. Hayo yamesemwa na ikulu ya Marekani mjini Washington.

Maafisa wamesema idadi ya vifo kutokana na kimbunga Helene imeongezeka hadi kufikia 88 jana Jumapili, huku kaunti moja pekee katika jimbo la North Carolina ikiripoti vifo 30. Waokoaji wamekuwa wakipambana kuwafikia watu wanaohitaji msaada kote katika eneo la kusini mashariki la Marekani.

Kimbunga hicho kimesababisha uharibifu katika majimbo kadhaa yakiwamo Florida, Georgia, North Carolina, South Carolina na Tennessee, huku upepo mkali na mvua kubwa zikiiwacha miji katika uharibifu mkubwa, barabara zikikumbwa na mafuriko na mamilioni ya watu wakiachwa bila umeme.