1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMarekani

Biden kuzungumza na Waziri Mkuu wa Israel Netanyahu

4 Aprili 2024

Rais Joe Biden wa Marekani atafanya mazungumzo kwa njia ya simu na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu baadaye leo mchana.

https://p.dw.com/p/4ePGY
Israel, Tel Aviv | Joe Biden
Rais Joe Biden wa MarekaniPicha: Evan Vucci/AP Photo/picture alliance

Mazungumzo hayo yanafanyika siku tatu tangu Israel ilipofanya shambulizi lililosababisha vifo vya wafanyakazi 7 wa kutoa misaada ndani ya Ukanda wa Gaza.

Afisa mmoja wa Ikulu ya Marekani amesema yumkini rais Biden atayatumia mazungumzo hayo kumtaka Netanyahu kuwalinda zaidi wafanyakazi wa mashirika ya misaada pamoja na kuruhusu misaada mingi ya kiutu kuingia Gaza.

Utawala wa Biden tayari umeirai Israel kufanya uchunguzi wa kina na wa uwazi juu ya shambulio hilo la mwanzoni mwa wiki lililowaua wafanyakazi wa shirika linalosambaza chakula huko Gaza la World Central Kitchen.

Mauaji ya wafanyakazi wa shirika hilo yamezusha lawama kutoka kile pembe ya dunia na rais Biden mwenyewe alisema amefadhaishwa na mkasa huo lakini hakutoa ishara  za kubadili uungaji mkono wa utawala wa Washington kwa Israel.