Biden na Modi wafanya mazungumzo juu ya vita nchini Ukraine
27 Agosti 2024Modi ameandika katika mtandao wa kijamii wa X kwamba amezungumza na Biden kuhusu "uungaji mkono kamili” wa India katika kurudisha amani na utulivu nchini Ukraine.
Ikulu ya Marekani imeeleza kuwa inakaribisha jukumu la Modi kujaribu kurudisha amani nchini Ukraine.
Soma pia: Modi amrai Zelensky kukaa mezani kumaliza vita na Urusi
Msemaji wa baraza la usalama la kitaifa John Kirby amewaambia waandishi wa habari kuwa, Marekani inaunga mkono nchi yoyote inayojaribu kumsaidia Rais Volodymyr Zelensky kuelekea kupatikana kwa amani.
Ziara ya Modi mjini Kyiv imetokea baada ya kiongozi huyo wa India kukutana na Putin mjini Moscow mwezi uliopita.
Zelensky alimkosoa Modi kwa ziara yake mjini Moscow, iliofanyika siku moja wakati Urusi ilipofanya mashambulizi ya makombora nchini Ukraine na kusababisha vifo vya watu kadhaa.