JamiiMexico
Biden, Trudeau na Lopez kujadili uhamiaji nchini Mexico
9 Januari 2023Matangazo
Huku biashara na masuala ya mazingira yakiwa yanatarajiwa kujadiliwa katika mkutano huo utakaomjumuisha pia Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau, Biden ameyapa kipau mbele masuala ya ongezeko la uhamiaji na ulanguzi wa madawa ya kulevya katika ziara yake hiyo ya kwanza nchini Mexico tangu achukue uongozi.
Alipokuwa njiani kuelekea Mexico kwa mkutano huo wa kilele uliopewa jina "Three Amigos" au mkutano wa kilele wa marafiki watatu, Biden alisimama kwa masaa kadhaa katika mji wa El Paso huko Texas, mji unaopakana na Mexico na unaokabiliwa na tatizo hilo la uhamiaji.
Aliyekuwa rais wa zamani wa Marekani Donald Trump aliwahi kutangaza mpango wa kujenga ukuta kwenye mpaka kati ya Mexico na Marekani.