1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blinken aelekea Brussels kwa mazungumzo kuhusu Ukraine

12 Novemba 2024

Antony Blinken anaelekea mjini Brussels kwa mazungumzo na washirika wake wa Ulaya huku kukiwa na wasiwasi kwamba rais mteule Donald Trump anaweza kuitelekeza Ukraine katika vita vyake na Urusi.

https://p.dw.com/p/4mvhj
Antony Blinken
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Antony BlinkenPicha: dts-Agentur/picture alliance

Katika ziara yake ya kwanza nje ya nchi tangu Trump alipochaguliwa tena, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken ataizuru Brussels kabla ya kuelekea Peru na Brasil baadae wiki hii. 

Vikosi vya Ukraine vyakabiliana na askari 50,000 wa Urusi katika mkoa wa Kursk

Katika mikutano na viongozi wa jumuiya ya kujihami ya NATO na Umoja wa Ulaya, Blinken atajadili uungaji mkono kwa Ukraine katika ulinzi wake dhidi ya uvamizi wa Urusi. 

Trump amekuwa mkosoaji wa msaada wa Biden kwa Ukraine na hivyo kuzusha mashaka ya kwamba huenda akaacha kuiunga mkono serikali ya Volodymyr Zelensky.