1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Blinken afanya mazungumzo na rais wa Mamlaka ya Palestina

Sylvia Mwehozi
11 Januari 2024

Mwanadiplomasia mkuu wa Marekani Antony Blinken ameeleza kuwa Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmud Abbas, anakusudia kufanya mageuzi katika uongozi ili kuunganisha tena Gaza iliyokumbwa na vita na Ukingo wa Magharibi.

https://p.dw.com/p/4b6Jb
Antony Blinken na Mahmud Abbas
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken na Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmud AbbasPicha: Evelyn Hockstein/REUTERS

Mwanadiplomasia mkuu wa Marekani Antony Blinken ameeleza kuwa Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmud Abbas, anakusudia kufanya mageuzi katika uongozi wake ili kuunganisha tena Gaza iliyokumbwa na vita na Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.

Blinken aliyasema hayo baada ya kukutana na rais wa Palestina katika ziara yake ya nne ya Mashariki ya Katiyenye lengo la kuzuia vita vya Israel na Hamas kusambaa zaidi.

Shirika la habari la Palestina Wafa limeripoti kwamba, Rais Abbas alimweleza Blinken haja ya kuzuia uchokozi wa Israel dhidi ya watu wa Palestina na Ukingo wa Magharibi.

Blinken amesisistiza kuwa Washington inaunga mkono hatua za wazi kuelekea kuundwa kwa taifa la Palestina, ambalo ni lengo la muda mrefu linalopingwa na serikali ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu. Blinken ameendelea na ziara yake huko Bahrain.