1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blinken airai Rwanda kuwakabili waasi Kongo

16 Desemba 2022

Waziri wa Mambo ya kigeni Marekani Antony Blinken ameirai Rwanda kutumia ushawishi wake kuwadhibiti waasi wa M23 dhidi ya mbele nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo

https://p.dw.com/p/4L37j
USA | US-Afrika Gipfel | Antony blinken und Felix Tshisekedi
Picha: Evelyn Hockstein/Pool via AP/picture alliance

Waziri wa Mambo ya kigeni Marekani Antony Blinken ameirai Rwanda kutumia ushawishi wake kuwadhibiti waasi wa M23 dhidi ya mbele nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Blinken amewaambia waandishi wa habari pembezoni mwa mkutano wa kilele kati ya Marekani na Afrika kuwa katika wakati waasi wa M23 wameonesha nia ya kusitisha mapigano na kujiondoa kwenye maeneo wanayoyashikilia, uungaji mkono wa Rwanda ni jambo muhimu.

Kwenye mkutano huo, Blinken alifanya mazungumzo na rais wa Kongo Felix Tshisekedi ambaye utawala wake unailaumu Rwanda kuwaunga mkono waasi wa M23.

Hata hivyo Blinken hakukutana na rais Paul Kagame wa Rwanda, ambayo hivi karibuni aliashiria nia ya kutaka kuwa na mazungumzo ya ngazi ya juu na Marekani.