Blinken anarejea tena Mashariki ya Kati kutafuta amani
10 Juni 2024Matangazo
Mwanadiplomasia huyo wa juu wa Marekani, anafanya ziara yake ya nane katika eneo hilo tangu vita vilipozuka, akitarajiwa kuanza safari hiyo nchini Misri na baadae leo hii kadhalika kuelekea Israel.
Amepangiwa kufanya mazungumzo ya ndani, kwanza mjini Cairo na Rais Abdel Fattah al-Sisi, mshirika mkuu wa Marekani katika juhudi za amani na baadae mjini Jerusalem na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.
Blinken amepanga ziara hiyo ili kulitolea msukumo zaidi pendekezo hilo lilitangazwa Mei 31 na Rais Joe Biden ambaye ameongeza juhudi za kumaliza vita ambavyo vimewaathiri vibaya raia na kumvuruga kisiasa kabla ya uchaguzi wa Novemba wa Marekani.