1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Blinken atua Beijing kwa ziara ya ngazi ya juu

18 Juni 2023

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Anthony Blinken ameanza ziara yake ya ngazi za juu nchini China kwa mazungumzo na mwenzake Qin Gang mjini Beijing.

https://p.dw.com/p/4SjQV
China | Marekani  Antony Blinken
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Anthony Blinken na mwenzake wa China Qin Gang mjini Peking.Picha: LEAH MILLIS/REUTERS

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Anthony Blinken ameanza ziara yake ya ngazi za juu nchini China kwa mazungumzo na mwenzake Qin Gang mjini Beijing.

Pande zote mbili zimeelezea matumaini ya kuboresha mawasiliano na kuzuia migogoro, licha ya tofauti zilizopo baina ya madola hayo mawili yenye nguvu kubwa ya kiuchumi ulimwenguni katika masuala kadhaa kuanzia ya kibiashara hadi teknolojia na usalama wa kikanda.

Kabla ya ziara hiyo ya Blinken, msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China Wang Wenbin alisema Marekani inatakiwa kuheshimu maswala ya msingi ya China na kuacha dhana potofu ya kutaka kulidhoofisha taifa hilo.

Blinken anakuwa afisa wa ngazi ya juu kabisa wa Marekani kuzuru China tangu Rais Joe Biden alipoingia madarakani na waziri wa kwanza wa mambo ya nje kufanya ziara hii katika kipindi cha miaka mitano.