Blinken akumbusha "uwajibikaji" kati ya Marekani na China
25 Aprili 2024Blinken amesema mataifa hayo yanawajibika sio tu kwa watu wao bali ulimwengu mzima na kwa maana hiyo wanalazimika kusimamia uhusiano baina yao kwa uwajibikaji. Blinken amesema hayo mjini Shanghai alipokutana na kiongozi wa Chama cha Kikomunisti.
Blinken yuko ziarani China akilenga kusaka suluhu ya masuala kadhaa yanayotishia utulivu wa kimahusiano baina ya mataifa hayo.
Atakutana pia na viongozi wa kibiashara kabla ya kwenda Beijing kesho Ijumaa kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, na pengine atakutana na Rais Xi Jinping.
Wasiwasi kati ya mataifa hayo mawili yenye nguvu kubwa kiuchumi ulimwenguni yameimarika kwa kiasi fulani tangu ziara yake ya mwezi Juni, ambapo hadi wakati huo alikuwa afisa wa ngazi za juu kabisa wa Marekani kuzuru China baada ya miaka mitano.