1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Blinken na Erdogan wajadili mzozo wa Gaza mjini Istanbul

6 Januari 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amekutana na rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki mjini Istanbul na kuzungumzia vita vya Ukanda wa Gaza na maombi ya Uturuki ya kuuziwa ndege za kivita za Marekani.

https://p.dw.com/p/4avgl
Antony Blinken (kushoto) akisalimiana na rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken (kushoto) akisalimiana na rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki mjini Istanbul.Picha: Murat Cetinmuhurdar/Turkish Presidency/Anadolu/picture alliance

Mkutano wake na Erdogan unafuatia ule alioufanya na mwenzake wa Uturuki Hakan Fidan ambapo wamejadili hali ya kiutu huko Ukanda wa Gaza na mchakato wa kuikaribisha Sweden ndani ya Jumuiya ya Kujihami ya NATO.

Blinken anatazamiwa jioni hii kuelekea nchini Ugiriki kwa dhamira ya kutuliza wasiwasi wa viongozi wa taifa hilo juu ya mpango wa Washington wa kutaka kuiuzia Uturuki ndege mamboleo za kivita chapa F-16. Ugiriki ambayo ni hasimu mkubwa wa Uturuki inapinga mauzo hayo.

Hapo kesho mwanadiplomasia huyo wa Marekani ataelekea Mashariki ya Kati kwa ziara nyingine ya kujaribu kupunguza mivutano inayotishia kuugeuza mzozo wa Gaza kuwa wa kanda nzima.