1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blinken ziarani Afrika Magharibi

22 Januari 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ameanza ziara ya wiki moja magharibi mwa Afrika kuangazia kuimarisha urafiki na mataifa hayo katikati ya kuzorota kwa usalama katika ukanda wa Sahel.

https://p.dw.com/p/4bWwC
Marekani | Sahel |  Antony Blinken
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken.Picha: Denis Balibouse/REUTERS

Blinken anaanzia ziara yake Cape Verde, kabla ya kuelekea Ivoary Coast, Nigeria na Angola, ikiwa ni ziara ya kwanza Afrika katika kipindi cha miezi 10.

Msaidizi wa Blinken kwenye masuala ya Afrika, Molly Phee, amesema mwanadiplomasia huyo ataangazia namna ya kusaidia nchi hizo kuimarisha jamii zao na kuzuia kuongezeka kwa kitisho cha ugaidi katika ukanda wa Sahel.

Amesema atayahimiza mataifa kutilia kipaumbele usalama wa raia wakati wa operesheni za kijeshi na kuhamamsiah haki za binaadamu na maendeleo ya kijamii na hasa kwenye jamii zilizo katika mazingira hatarishi.