Boeing 737 kurejea tena angani baada ya kuzuiliwa miezi 20
19 Novemba 2020Kulingana na mamlaka ya usafiri wa anga FAA, kuachiwa kwa ndege hizo kuanza safari zake tena kunatokana na utafiti binafsi uliofanywa kwa ndege hizo na mamlaka za ndege duniani kote. Katika vidio iliokuwa na ujumbe huo, mkurugenzi wa FAA Steve Dickson amesema ana imani kubwa na ndege hizo kufikia kiwango cha kuiacha familia yake kusafiri nazo
Ndege hizo zilipigwa marufuku ya kuendelea na shughuli zake baada ya kupata ajali mbaya zilizosababisha vifo vya watu 346 mwaka 2018 na 2019.
Mwezi Oktoba mwaka 2018, ndege ya shirika la Lion Air nambari 610 ilianguka baharini muda mfupi baada ya kupaa angani na kusababisha vifo vya watu 189. Miezi mitano baadae ndege nambari 302 ya shirika la Ethiopia ilianguka ilipokuwa inaelekea mjini Nairobi na kusababisha vifo vya watu 157. Boeing pamoja na mamlaka ya FAA zote zilishambuliwa huku wakosoaji wakisema Boeing ilikuwa inaangalia faida inayopata kuliko maisha ya wateja wake.
Sababu ya ajali hizo mbili zilielezewa kuwa mifumo mibovu ya ndege zote mbili, zilizopaswa kuifanya ndege hiyo kupaa vizuri angani lakini badala yake iliielekeza ndege kuanguka. Mamlaka ya FAA iliilazimisha ndege hiyo kurekebisha mifumo yake kabla ya kuruhusiwa kuendelea na safari zake.
Shirika hilo la ndege aina ya Boeing 737 Max lilikubaliana na matwakwa hayo kutokana na umuhimu uliopo wa ndege hizo kurejea angani na umuhimu wa kujenga tena uaminifu mingoni mwa wasafiri wake na kutosahau maisha ya wale walioangamia kutokana na ajali zilizosababishwa na ndege hizo.
Boeing, ambayo mara moja ilimbadilisha mkurugenzi wake mkuu na maafisa wengine wa juu kufuatia mgogoro huo pia imeathirika pakubwa katika ndege zake ndogo kufuatia janga la virusi vya corona.
Hakuna aliyenusurika kwenye ajali ya ndege ya UkraineHata hivyo familia iliyopoteza wapendwa wao iliishutumu hatua ya kuwafuta kazi wafanyakazi wa juu wa ndege hiyo ya Boeing. Michael Stumo mzazi aliyempoteza binti yake katika ajali ya ndege ya Ethiopia mwezi Machi mwaka 2019 amesema usiri wa FAA unamaanisha hawawezi kuiamini tena Boeing 737 Max kuwa salama. Ajali nyengine iliowauwa wengi ni ile ya kampuni ya ndege ya Lion ilioanguka Indonesia Oktoba mwaka 2018.
Stumo anasema waliambiwa ndege hiyo ni salama mwaka 2017 na baada ya ajali ya mwaka 2018 imani na ndege hiyo ikaondoka.
Lakini katika kurejesha imani hiyo Boeing imefanya marekebisho yote yaliohitajika kwa ndege zake zote. Mkuregenzi wa FAA Steve Dickson amesema mabadiliko yaliofanywa hayawezi kusababisha ndege hiyo kupata ajali kama zile zilizotokea awali.
Ndege hizo aina ya Boeing hata hivyo zimeripoti kupata hasara kubwa katika robo nne ya mwaka na mgogoro wa max wameipa hasara ya dola bilioni 20.
Kwa sasa bado FAA inapaswa kuidhinisha mafunzo ya marubani kwa ndege hizo kabla ya kuendelea rasmi na safari zake zinazotarajiwa kuanza katika robo ya pili ya mwaka 2021.