1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BONN : Egaland ataka kukomeshwa ubakaji Congo

9 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDEC

Mkuu wa masuala ya kibinaadamu wa Umoja wa Mataifa Jan Egeland ametowa wito wa kukomeshwa kwa vitendo vya ubakaji vinavyowasibu wanawake katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo nchi ilioathirika na vita.

Akizungumza na idhaa ya Kingereza ya Radio Deutsche Welle Egeland amesema wahusika wengi wa unyama huo ni wanajeshi wa serikali.Egeland ambaye hapo Ijumaa alikamilisha ziara yake yake ya siku tatu katika maeneo ya mashariki mwa Congo amesema wanawake katika eneo hilo wanaendelea kuteseka sana kutokana na vitendo vya kulazimishwa ngono.

Idadi halisi ya vitendo hivyo vya ubakaji haijulikani lakini maafisa wa hospitali wanaendelea kuripoti kwamba idadi kubwa ya wanawake wanaendelea kuripoti juu ya kushambuliwa kingono hususan mashariki ya Congo ambapo wapiganaji wanamgambo na wanajeshi wa serikali wanaendelea kuwashambulia raia.