MigogoroKosovo
Borell alaani mauaji ya polisi huko Kosovo
24 Septemba 2023Matangazo
Katika taarifa yake, Borrell amesema kuwa ukweli wote kuhusu shambulio hilo unahitaji kubainishwa na aliyehusika kuwajibishwa.
Borrell ameongeza kuwa maisha zaidi ya watu wasio na hatia yamo hatarini katika mapigano yanayoendelea nchini humo hasa katika maeneo ya karibu na Banjska, na kutoa wito wa kusitishwa kwa mashambulizi hayo mara moja.
Borrell amesema pia kuwa Ujumbe unaosimamia utawala wa sheria wa Umoja wa Ulaya EULEX unawasiliana na mamlaka nchini Kosovo pamoja na ujumbe wa kulinda amani wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO, huku akirejelea wito wa Umoja wa Ulaya na mataifa wanachama wa kusitisha uhasama katika eneo la Kaskazini mwa Kosovo, lenye idadi kubwa ya raia wa jamii ya Waserbia.