1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Borrell atoa rai kutuliza ghasia Mashariki ya Kati

3 Februari 2024

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell ametoa wito pande hasimu kuzuia kuongezeka mvutano huko Mashariki ya Kati, baada ya Marekani kuyashambulia makundi yanayohusishwa na Iran nchini Iraq na Syria.

https://p.dw.com/p/4c0jM
Albanien Der Hohe Vertreter der EU für Außen- und Sicherheitspolitik, Josep Borell, auf der gemeinsamen Pressekonferenz in Tirana
Picha: Press Office, Albania Premiership

Borrell ametoa wito huo mjini Brussels Ubelgiji wakati wa mkutano wa mawaziri wa mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya, akisema kila mmoja anapaswa kujizuia ili kuepuka mvutano huo kuwa mkubwa. Marekani ilianzisha mashambulizi ya anga dhidi ya vikosi vya Iran na wanamgambo ambao ni washirika wa Tehran katika mataifa ya Iraq na Syria siku ya Ijumaa. Rais Joe Biden wa Marekani ameapa mashambulizi zaidi ya kulipiza kisasi kufuatia shambulizi baya la droni lililowaua wanajeshi watatuwa Marekani kwenye kambi yake huko Jordan.