Boti yazama Mto Kongo na kuwauwa watu 22
18 Desemba 2024Matangazo
Afisa wa serikali ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba boti hiyo ilikuwa imebeba takriban abiria 100 wakati ilipozama jana Jumanne katika jimbo la Mai-Ndombe, magharibi mwa nchi hiyo.
Miongoni mwa wahanga wa ajali hiyo ya boti ni wanawake 15, wanaume watano na watoto wawili.
Ajali za boti hutokea mara kwa mara nchini Kongo ambako vyombo hivyo vya baharini na vya zamani vinatumika kwa ajili ya safari kati ya kijiji kimoja hadi kingine, na mara nyingi hubeba watu kushinda uwezo wake.
Mnamo mwezi Oktoba, watu 78 walikufa baada ya boti iliyokuwa imebeba abiria 278 kuzama kwenye ziwa Kivu mashariki mwa nchi hiyo.