1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Botswana kuwa mthibitishaji katika marufuku ya almasi

28 Novemba 2024

Botswana, moja wapo kati ya nchi wazalishaji wakubwa wa almasi barani Afrika, itaungana na Eneo la kudhibiti vito vya Almasi barani Ulaya katika makao yake mjini Antwerp

https://p.dw.com/p/4nWXP
Indien Surat Diamanten
Picha: PUNIT PARANJPE/AFP/Getty Images

Hii ni baada ya kupata uungwaji mkono mkubwa wa kuingizwa kwenye kundi la nchi zilizo na jukumu la kuthibitisha uchimbaji wa Almasi ghafi na kuzisafirisha Almasi hizo kwenda kwenye mataifa ya G7 ambayo yalipiga marufuku uagizaji wa Almasi kutoka Urusi.

Kushirikiswa Botswana katika mfumo huo mpya wa ufuatiliaji kunalenga kushughulikia wasiwasi kuhusu usawa wa kiuchumi wa wazalishaji wa barani Afrika, zikiwemo nchi za Angola na Namibia.

Mfumo huo wa ufuatiliaji ulipaswa kuanza mwezi Septemba mwaka huu, lakini Umoja wa Ulaya  umeahirisha utekelezwaji wake hadi Machi mwaka ujao wa 2025.