1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBotswana

Rais Mokgweetsi Masisi kusaka muhula wa pili madarakani

28 Oktoba 2024

Botswana itafanya uchaguzi wa bunge Jumatano wiki hii, ambao utaamuwa ikiwa chama tawala cha Bostwana Democratic, BDP kitafanikiwa kendeelea kubakia madarakani.

https://p.dw.com/p/4mJ7p
Rais wa Botswana, Mokgweetsi Masisi anazungumza na DW
Rais wa Botswana, Mokgweetsi Masisi anazungumza na DWPicha: DW

Rais Mokgweetsi Masisi anataka kutafuta muhula wa pili na wa mwisho wa kukaa madarakani, japo uchaguzi huo sio moja kwa moja wa kumchagua rais.

Wapiga kura watafanya maamuzi ya kuwachagua wabunge ambao baadae watamchagua rais.

Chama tawala cha BDP kimehodhi siasa za Bostwana tangu ilipopata uhuru wake kutoka Uingereza mwaka 1966.

Uchaguzi huo wa Jumatano unafanyika katikati ya kiwingu cha hali mpya ya mashaka ya kiuchumi kwenye nchi hiyo ambayo inategemea kwa kiasi kikubwa uchimbaji madini ya almasi.