1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBrazil

Brazil yapinga ukosoaji wa Marekani kuhusu uhusiano na Urusi

18 Aprili 2023

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergey Lavrov ameishukuru, Brazil kwa juhudi zake za kujaribu kusuluhisha mgogoro wa Ukraine. Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergey Lavrov ameishukuru Brazil kwa juhudi za kutafuta amani

https://p.dw.com/p/4QE8Q
Brasilien Außenminister Lawrov bei Mauro Vieira
Picha: Ton Molin/AA/picture alliance

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergey Lavrov ameishukuru, Brazil kwa juhudi zake za kujaribu kusuluhisha mgogoro wa Ukraine. Kwa upande wake Marekani imeilaumu Brazil juu ya msiamo wake kuhusu umavizi wa Urusi nchini Ukraine na imesema nchi hiyo ya Amerika ya Kusini inazifuata propaganda za Urusi na China.

Soma pia: Lula ahimiza upatanishi wa pamoja kumaliza mzozo nchini Ukraine

Wakati huo huo mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa makubwa kiuchumi duniani, G7 wameonya leo Jumanne kwamba taifa lolote linalosaidia juhudi za vita vya Urusi dhidi ya Ukraine litakabiliwa na pingamizi kali.

Mawaziri hao wanaokutana nchini Japan, wamesisitiza msimamo wao wa kukabiliana na taifa lolote litakalo isaidia Urusi kukwepa vikwazo na kuipa silaha.