BRUSSELS: Solana aikaribisha serikali mpya ya Palestina
16 Machi 2007Kiongozi wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya, Javier Solana, ameikaribisha serikali mpya ya umoja wa taifa ya mamlaka ya Palestina.
Hata hivyo kiongozi huyo amesisitiza kwamba ni mapema mno kuamua juu ya kuanza kupeleka tena misaada ya moja kwa moja kwa Wapalestina.
Umoja wa Ulaya umesema utakuwa tayari kuondoa kiwazo dhidi ya mamlaka ya Palestina ikiwa itakubali kulaani machafuko, kuitambua Israel na kuheshimu mikataba ya amani iliyofikiwa hapo awali baina ya Israel na Palestina.
Isreal imeukosoa msimamo wa serikali mpya ya kitaifa ya Palestina ambao haujumulishi kulitambua taifa hilo la kiyahudi.
Jana waziri mkuu mteule, ambaye pia ni kiongozi wa chama cha Hamas, Ismael Haniyeh, aliwasilisha serikali yake ya umoja wa taifa kwa rais wa mamlaka ya Palestina, Mohmoud Abbas wa chama cha Fatah.