Brussels.Solana afurahishwa na kauli ya kiongozi wa Palestina.
12 Septemba 2006Matangazo
Mkuu wa sera za nn’je wa umoja wa Ulaya Javier Solana amefurahishwa na kauli ya jana iliyotolewa na liongozi wa Palestina ya kuunda serikali ya muungano.
Katika maelezo yake, Solana amesema kuwa, maendeleo hayo yanaweza yakaharakisha harakati za amani mashariki ya kati.
Hata hivyo, kama ilivyo kwa Marekani na Israel, umoja wa Ulaya umeutaka uongozi wa sasa wa Palestina chini ya chama cha Hamas, kuitambua Israel, kusimamisha mapigano na kukubali mpango wa amani.
Lakini kundi hilo la wanamgambo wa kiislamu limesema katu halitaitambua Israel.
Nchi za magharibi zitaendelea kuzuia misaada kwa Palestina hadi Hamas watakapoitambua Israel.