BUNDESLIGA: BAYERN MÜNICH KABLA CHANGAMOTO YA KESHO NA REAL MADRID KOCHA WA ZAMANI WA BRAZIL FELIPE SCOLARI AUIUNGAMKONO MOROCCO KUANDAA KOMBE LA KWANZA LA DUNIA BARANI AFRIKA 2010
23 Februari 2004Katika Bundesliga-Ligi ya Ujerumani,ushindi wazi kwa mabingwa wa Ujerumani Bayern munich mwishoni mwa wiki,ungewatia moyo sana kwa zahama yao ya hapo kesho ya champions League-kombe la klabu bingwa barani Ulaya kati yao na mahasimu wao wakubwa Real Madrid ya Spain.badala yake lakini,Munich iliondokea na ushindi chupu-chupu wa bao 1:0 dhidi ya Hamburg wa bao 1:0.
Hatahivyo, ushindi huo ulipumnguza mwanya kutoka kileleni iliko Werder Bremen kutoka pointi 9 kuwa 7,kwani viongozi wa ligi Bremen wali mudu mara hii sare bao 1:1 na Schalke 04. Stuttgart, timu ya pili ya Ujerumani katika champions League-kombe la klabu-bingwa barani Ulaya,wao walizabwa bao 1:0 na kaiserslauten .Stuttgart inacheza keshokutwa nyumbani na Chelsea katika duru ya kutoana ya champions league-kombe la klabu-bingwa barani Ulaya. Mabingwa wa 1997 wa Kombe hilo la Ulaya-Borussia Dortmund waliondoka jana na ushindi wa bao 1:0 dhidi ya FC Cologne inayoburura mkia wa Ligi.Kwa kweli,Cologne ndio iliokua timu bora lakini bao walitia Dortmund. Ewerthon kutoka Brazil ndie alieufumania mlango wa FC Cologne mnamo dakika ya 25 ya mchezo.
Hertha Berlin, iliokua klabu pekee ya Bundesliga 2001,ilioingia uwanjani bila ya mchezaji wa kiafrika, imemuajiri mshambulizi wa Enyimba-klabu bingwa ya Afrika Michael Ochei.Ochei amefungishwa mkataba wa miaka 2 na Berlin. LUIZ FELIPE SCOLARI, alieiongoza Brazil kutwaa kombe lililopita la dunia huko Japan,jana aliiungamkono Morocco kuwa ndio inayofaa kuandaa Kombe la dunia 2010.Scolari ambae sasa anaifunza Ureno kwa Kombe lijalo la Ulaya la mataifa amesema kwamba Morocco ina kila kitu tayari kwa kuandaa Kombe hilo.Mbrazil huyo na ukoo wake walikuwa wenyeji wa timu inayofanya kamepni kwa Morocco mwishoni mwa wiki na alizuru miji yote 2 Casablanca na Marrakesh na huko alijionea vciwanja na zana nyengine.
Morocco inashindana na Afrika kusini,Misri,Libya na Tunisia kuania haki ya kuandaa kombe la kwanza la dunia barani Afrika 2010.uamuzi wapi Kombe hilo litachezwa utakatwa Mei mwaka huu mjini Paris. Kocha wa simba wa nyika katika kombe lililopita la dunia na la Afrika nchini Tunisia, mjerumani Winfried Schäfer atakua sasa kocha mpya wa Misri-kwa muujibu wa gazeti la cairo, AL GOUMHORIA. Schäfer anajaza hapo pengo lililoachwa na kujiuzulu kwa Mhsoen salah baada ya mafiraouni wa Misri kutimuliwa nje ya kombe la afrika duru ya kwanza tu huko Tunis.
Schäfer nae hakutimiza shabaha ya simnba wa nyika kutwaa Kombe la Afrika mara ya tatu mfululizo au mara ya 5 kwa jumla. Kama Misri na Ghana, kamerun imetawazwa mabingwa wa Afrika mara 4. Kinyume na makocha hao wawili Schäfer na Mohsen, kocha wa Tunisia,mfaransa Roger Lemerre,atabakia kocha wa mabingwa wapya wa Afrika-Tunisia hadi mwaka 2006-mwaka wa Kombe la dunia -Ujerumani.
Mshambulizi wa Afrika kusini Beni McCarthy,alieacha kuichezea timu ya taifa kufuatia mivutano kadhaa na timu hiyo, ndie anaeongoza sasa katika kutia mabao mengi katika Ligi ya ureno.McCathy ametia mabao 13 kwa klabu yake ya FC Porto. KINYAN'GANYIRO CHA KUANIA TIKETI ZA OLIMPIK:
Wiki tu baada ya kutawazwa mabingwa wapya wa Afrika, timu ya chipukizi ya Tunisia -chini ya umri wa miaka 23 imepiga hatua kukaribia kutia mfukoni tiketi yake kwa dimba la Olimpik huko Athens,Ugiriki.Tunisia imeilaza Misri kwa mabao 2:0. Mwezi ujao,Tunisia itafunga safari hadi Dakar,kupambana na Senegal kabla haikumaliza mpambano wake wa mwisho na Nigeria-mpambano utakaokumbusha changamoto yao ya nusu-finali katika Kombe la Afrika. Nigeria ilkiizaba Senegal mabao 2:0 wakati simba wa nyika kamerun walinguruma mbele ya Tembo wa Ivory Coast kwa mabao 2:0.Morocco iliizaba Uganda mabao5:0 mjini Rabat wakati Angola imeitimua Ethiopia kwa mabao 4:0 mjini Luanda. Ghana imeilaza algeria 2:0 na kuparamia wao kileleni mwa kundi D.