1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bundesliga kuendelea wikiendi baada ya mechi za kimataifa

Sylvia Mwehozi
15 Oktoba 2020

Baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa, ligi ya kandanda ya Ujerumani Bundesliga inaendelea tena mwishoni mwa juma hili.

https://p.dw.com/p/3jxzp
Bundesliga I TSG Hoffenheim - BVB Dortmund

RB Leipzig ambao wanaongoza ligi kwa pointi 7 watasafiri na kuwafuata Augsburg ambao wako nafasi ya pili wakiwa na pointi zilezile lakini kwa tofauti ya goli huku nafasi ya tatu ikishikiliwa na Eintracht Frankfurt.

Mabingwa watetezi Bayern Munich wako nafasi ya nne. Borussia Dortmund watakuwa na matumaini ya kuondosha rekodi yao mbaya ya hivi karibuni wakati watakapomenyana na Hoffenheim na siku ya Jumapili Schalke watakuwa wakijaribu kusaka pointi yao ya kwanza nyumbani watakapowakaribisha Union Berlin, baada ya kuanza vibaya msimu huu.

Freiburg watakutana na Werder Bremen, Hertha Berlin na VfB Stuttgart wakati Mainz wanacheza na

Bayer Leverkusen. Pia Cologne wanawakaribisha Frankfurt siku ya jumapili.

Ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona nchini Ujerumani linamanisha kwamba huenda mechi zikachezwa bila ya mashabiki kuwepo uwanjani. "Ni wazi tumesikitika tuliposikia taarifa hizi" alisema  Andre Hahn winga wa FC Augsburg, akiongeza kuwa wana matumaini mechi zinazokuja mashabiki wataweza kuruhusiwa tena kuingia viwanjani.