1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bundesliga: Utata wa marefa na makocha

27 Februari 2016

Bruno Labaddia na Thomas Schaaf wote wanatumai kuwa kunaweza kuwa na mawasiliano bora baina ya makocha waBundesliga na marefa kutokana na hatua ya kupigwa marufuku ya mechi tatu Roger Schmidt baada ya kujibizana na refa

https://p.dw.com/p/1I3Ns
Bundesliga Bayer Leverkusen - Borussia Dortmund Felix Zwayer Roger Schmidt
Picha: Getty Images/AFP/P. Stollarz

Shirikisho la kandanda Ujerumani – DFB lilimfungia kocha wa Leverkusen Schmidt kuhudhuria michuano mitatu ijayo ya ligi, na kutozwa faini ya euro 20,000.

Ilikuwa adhabu yake kwa kukataa kutii amri ya refarii kuondoka katika eneo la benchi ya kiufundi wakati wa mchuano mkali wa walioshindwa moja bila dhidi ya Borussia Dortmund Jumapili iliyopita. Alijibizana na refarii Felix Zwayer kutokana na goli la Pierre-Emerick Aubameyang la dakika ya 64 katika uga wa BayArena, ambalo lilifungwa baada ya wageni BVB kupiga mkwaju wa freekick mbali sana na eneo ambalo ilistahili kupigwa.

Schmidt mwenye umri wa miaka 48 amekubali adhabu yake na anasema alikosea kwa kushikwa na hasira lakini kocha wa HAMBURG Labbadia na mwenzake wa Hanover Schaaf wanasema wanamwonea huruma.

Labaddia anasema Schmidt ameomba radhi mara 14,000 lakini hakuna anayezungumza kuhusu mkwaju wa freekick uliopewa Dortmund kwa njia ya utata.

Anasema anatumai kuwa DFB sasa itachukua hatua ya kuimarisha mawasiliano baina ya makocha na marefa maana mapendekezo yanayotolewa na makocha yameonekana kupuuzwa kwa muda mrefu.

Schaaf aliyaunga mkono matamshi hayo, akisema ipo haja ya kuwapo mazungumzo. Anasema hadi kufikia sasa, hakuna mafanikio yaliyofikiwa kuhusu hilo. Anatumai kuwa pande zote mbili zinaweza kufikia makubaliano.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Mohamedn Dahman