1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUNDESLIGA

8 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CHai

Bundesliga-Ligi ya ujerrumani ilirudi uwanjani mwishoni mwa wiki kabla ya changamoto za kesho za champions League-kombe la klabu bingwa barabni Ulaya zitakazoamua hatima ya mabingwa wa Ujerumani-Bayern munich wanaokumbana na Anderlecht ya Ubelgiji: Katika Bundesliga-VFB Stuttgart imesalia kileleni licha ya kumudu suluhu 0-0 nyumbani na Hamburg jumamosi.stuttgart imerufusha rekodi yake ya kutoshindwa msimu huu katika Bundesliga hadi mechi 15 na sasa iko pointi 2 usoni mwa Ligi hii ikisubiri changamoto ya kati ya wiki hii na Manchester United ya uingereza katika kinyan'ganyiro cha champions League-kombe la klabu bingwa barani ulaya.

Mabingwa Bayern Munich wameangukia nafasi ya 4 wakiwa pointi 6 nyuma ya viongozi wa Ligi Stuttgart.hii inafuatia kumudu munich sare tu jumamosi katika mpambano wao na Bremen inayosimama wakati huu nafasi ya pili. Bayer Leverkusen ilioanza msimu huu kwa vishindo imeanza kupoteza kasi ,kwani jumamosi ilimudu nayo suluhu tu na mahasimu wao wa mtaani FC Cologne inayoburura mkia wa Ligi.Cologne baada ya kunyakua pointi 1 wiki moja kabla kutoka mabingwa bayern munich wamemudu tena kunyakua pointi 1 kutoka kwa Leverkusen katika juhudi yao ya kujikomboa kutoka mkiani mwa Ligi.

Nje ya Ujerumani, Real madrid ya Spain ilikata kiu cha miongo 2 na kuondoka na ushindi wa mabao 2-1 katika uwanja wa Nou camp wa FC barcelona.Ushindi huo umeiweka sasa Real kileleni mwa Ligi ya spain-Primera Liga.mabao ya Real yametiwa na wabrazil 2:Roberto carlos na Ronaldo.Bao la kufuta machozi la Barcelona ametia Patrick Kluivert kutoka Holland. AS Roma ya Itali imesawazisha pointi kileleni na AC Milan baada ya ushindi wao wa jumamosi dhidi ya Chievo wa mabao 3:0.

Barani Afrika, mabingwa wapya na wa mwisho wa Kombe la washindi barani Afrika ni Etoile du sahel ya tunisia ilioilaza kwea mabao 3-2 Julius berger ya Nigeria katika duru ya pili ya finali ya Kombe hilo.Mbele ya mashabiki 35.000 Etoile iliizaba Julius Berger mabao 3 bila jibu na hivyo kufuta ushindi wa duru ya kwanza wa Julius Berger wa mabao 2:0.

Julius Berger imeadhibiwa kwa madhambi iliofanya nyumbani mwishoni mwa wiki iliotangulia ilipopoteza nafasi kadhaa za kutia zaidi ya mabao 2. Kombe hili la washindi limechezwa kwa mara ya mwisho msimu huu.Kwa pigo hilo klabu ya kwanza ya Nigeria imetoka mikono mitupu katika finali ya Kombe la klabu za afrika.Matumaini pekee msimu huu kwa Nigeria kukata kiu cha miaka 35 yamesalia kwa Enyimba inayokumbana na Ismailia katika duru ya pili ya Kombe la klabu bingwa.