1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge la Australia lataka muasisi wa WikiLeaks arejeshwe

15 Februari 2024

Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese amesema anatumai patapatikana suluhisho la kesi ya miaka mingi inayomkabili muasisi wa tovuti ya kuvujisha nyaraka za siri ya WikiLeaks Julian Assange.

https://p.dw.com/p/4cRw5
Julian Assange | Wikileaks
Muasisi wa WikiLeaks Julian AssangePicha: Carmen Valino/El Pais/Newscom/IMAGO

 Hii ni baada ya wabunge kuongeza shinikizo dhidi ya Marekani na Uingereza kwa kupitisha muswada unaotoa wito kwa raia huyo wa Australia kuruhusiwa kurejea nyumbani.

Albanese ameyasema hayo bungeni siku chache kabla ya Mahakama Kuu ya Uingereza kusikiliza rufaa ya Assange wiki ijayo dhidi ya kurejeshwa nchini Marekani kwa tuhuma za ujasusi.

Amesema sio juu ya Australia kuingilia taratibu za kisheria za nchi nyingine, lakini inafaa kwa Australia kuwa na mtizamano wenye nguvu kwamba nchi hizo zinahitaji kuzingatia haja ya kulikamilisha suala hilo.

Soma pia:Albanese ataka mashtaka ya Assange yasitishwe

Assange amekuwa katika gwereza lenye ulinzi mkali la Belmarsh mjini London tangu alipokamatwa mwaka wa 2019.

Tangu hapo, aliishi katika ubalozi wa Equador mjini London kwa miaka saba ili kuepuka kuhamishiwa Sweden alikokabiliwa na mashitaka ya ubakaji na unyanyasaji wa kingono. Sweden iliutupilia mbali uchunguzi wa ubakaji mnamo 2019 kwa sababu muda mwingi ulikuwa umepita.