1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Congress imepitisha muswada wa kuiadhibu mahakama ya ICC.

5 Juni 2024

Bunge la Marekani jana limepitisha muswada utakaoipelekea Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC kuwekewa vikwazo, kwa kuomba waranti wa kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na maafisa wengine wa Israel.

https://p.dw.com/p/4geoG
Marekani | Capitol na Baraza la Wawakilishi katika ukungu
Ukumbi wa bunge la Marekani Novemba 4, 2022 huko Washington, DC.Picha: Samuel Corum/Getty Images

Muswada huo umepitishwa kwa kura 247 dhidi ya 155 za waliopinga. Kupitishwa kwa muswada huo ni hatua ya kwanza ya bunge la Congress kuonesha kutoridhishwa kwake na hazua ya mahakama hiyo ya kutaka waranti huo wa kukamatwa kwa viongozi wa Israel, jambo lililosababisha kuwepo kwa kipindi cha nadra cha umoja kwa Israel, licha ya migawanyiko iliyoko kuhusiana na vita hivyo vya Israel dhidi ya kundi la wanamgambo la Hamas. Muswada huo ulitarajiwa kupita katika Congress ila umewavutia wabunge wachache wa chama cha Democratic, jambo ambalo huenda likatilia shaka nafasi yake ya kupita katika Senate. Ikulu ya White House inaupinga muswada huo ikisema umevuka mipaka.