1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge la Kenya laidhinisha wanajeshi wao kupelekwa DRC

10 Novemba 2022

Bunge la taifa la Kenya limeridhia hatua ya kupeleka kikosi maalum katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kupambana na waasi.

https://p.dw.com/p/4JJEn
Kenia Verfassung
Picha: AP

Wanajeshi  903 wa kikosi hicho watahudumu kwenye eneo la mashariki na wametengewa bajeti ya shilingi bilioni 4.4 kwa muda wa miezi 6.

Zipo taarifa kuwa Kenya ambayo haina mpaka wa moja kwa moja na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo inaaminika zaidi kuliko majirani wa karibu.Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliafikiana mwezi Aprili kuunda kikosi cha pamoja cha kudumisha amani ya kikanda.

Kikosi hicho kijulikanacho kwa kifupi kama EACRN kinawajumuisha wanajeshi kutokea Burundi,Uganda, Sudan Kusini, Kenya na Tanzania imeahidi kupeleka kikosi chake baadaye.

Rwanda tayari ina wanajeshi wake kwenye maeneo ya mpakani.Wiki iliyopita Rais William Ruto aliwapa ridhaa rasmi wanajeshi wa Kenya kujiandaa kudumisha amani nchini Kongo.