Bunge la Uingereza kujadili Makubaliano mapya
17 Oktoba 2019Makubaliano hayo yamefikiwa masaa machache kabla ya mkutano wa kilele wa viongozi wa umoja wa ulaya unaotarajiwa kuyaunga mkono yale yaliyofikiwa lakini yataabidi yajadiliwe bungeni kuidhinishwa jumamosi inayokuja.
Waziri mkuu Boris Johnson aliyedhamiria kwa kila hali kuhakikisha nchi hiyo inaachana na Umoja wa ulaya hadi ifikapo mwisho wa mwezi huu, amesema amefikia maakubaliano mepya "yanayoipatia nchi yake udhibiti kamili".
Mwenyekiti wa halmashauri kuu ya Umoja wa ulaya Jean-Claude Juncker anayataja makubaliano hayo kuwa "ya haki na ya mizani sawa kwa Umoja wa ulaya na kwa uingereza na kwamba ni thibitisho la waajibu wao katika kutafuta ufumbuzi."
Makubaliano ni ushindi kwa Boris Johnson?
Makubaliano hayo ni ushindi kwa Boris Johnson aliyeingia madarakani mwezi Julai uliopita akiahidi kuitoa Uingereza kutoka Umoja wa Ulaya kuambatana na matokeo ya kura ya maoni ya mwaka 2016.
Hata hivyo makubaliano hayo yanaweza kupingwa yatakapowasilishwa mbele ya wabunge ili kuidhinishwa jumamosi inayokuja. Na ishara mbaya zimeshaanza kuonekana.
Sarafu ya Uingereza Pound imepungua thamani katika masoko ya hisa kutokana na wasi wasi kama bunge litayaidhinisha makubaliano hayo.Imepoteza asili mia 0.34 ikilinganishwa na dala ya Marekani.Wakatai huo huo sarafu ya euro imepanda thamani kwa asili mia 0.69.
Chama cha Ireland ya kaskazini ambacho wahafidhina wa chama cha Boris Johnson wanakitegemea bungeni,Democratic Unionist Party-DUP kinasema hakitoyaunga mkono makubaliano hayo kwasababu hayakidhi masilahi ya muda mrefu wa eneo lao.
Chama cha kihafidhina cha Boris Johnson hakidhibiti wingi wa viti katika bunge la viiti 650. Kimsingi panahitajika kura 320 ili makubalianao hayo yaweze kuidhinishwa jumamosi inayokuja. DUP kinakalia viti 10
Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha Labour, Jeremy Corbyn amewahimiza wabunge wayapinge makubaliano hayo."Makubaliano anayotuletea yataifanya uingereza isiwe na mtengamano na rasli mali yake kuuziwa makampuni ya Marekani.
Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/AFP/
Mhariri:Yusuf Saumu