1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge la Ulaya lamthibitisha Von der Leyen

16 Julai 2019

Ursula von der Leyen amethibitishwa na bunge la Ulaya kuwa rais mpya wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Jumanne, na kuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo wa fahari zaidi katika umoja huo, kwa kura 323-327.

https://p.dw.com/p/3MAi5
Frankreich Wahl zur EU-Kommissionspräsidentin | Ursula von der Leyen
Picha: Reuters/V. Kessler

Uthibitishwaji huo ulihitaji wingi wa kura 374 na waziri huyo wa ulinzi wa Ujerumani anaendoka alipita kwa ziada ya kura tisa.

"Najihisi mwenye heshima na furaha," alisema katika majibu yake ya kwanza. "Kazi iliyoko mbele yangu inanifanya kuwa mnyenyekevu."

Aliteuliwa nwa wakuu wa mataifa na serikali za Umoja wa Ulaya kama sehemu ya uteuzi jumla, lakini alihitaji kuungwa mkono na wabunge.

Aliibuka kama mgombea wa mwisho na wabunge wengi walikuwa na hasira kwa sababu hakuna kati ya mgombea wao alichaguliwa kwa wadhifa huo. "Ujumbe wangu kwenu nyote: Tushirikiane kwa kujenga," alisema.

Von der Leyen ameainisha ajenda yake ya kisiasa kwenye Ulaya ya kijani zaidi na yenye usawa wa kijinsia ambako utawala wa sheria unaendelea kuheshimiwa.

Frankreich Wahl zur EU-Kommissionspräsidentin | David-Maria Sassoli und Ursula von der Leyen
Rais mpya wa Halmashauri Kuu ya Ulaya Ursula von der Leyen akipongezwa na spika wa bunge la Ulaya David-Maria Sassoli, baada ya kura kuhusu uteuzi wake katika bunge la Ulaya mjini Strasbourg, Ufaransa, Julai 16, 2019.Picha: Reuters/V. Kessler

Kuidhinishwa kwake kulikuwa sehemu muhimu ya nyadhifa za juu ambazo wakuu wa Umoja wa Ulaya walikubaliana juu yake mapema mwezi huu.

Chini ya makubaliano hayo, kundi la waliberali la Renew Europe lilimpata waziri mkuu wa Ubelgiji Charles Michel kama rais wa Baraza la Ulaya na Wasoshalisti walipata nafasi ya juu katika bunge la Ulaya.

Chrsitine Lagarge kutoka Ufaransa alipendekezwa kuwa mkuu wa benki kuu ya Ulaya. Von der Leyen aliwamabia wabunge mjini Strasbourg Jumanne kuwa suala la jinsia litakuwa sehemu muhimu ya kazi yake.

"Nitahakisha usawa kamili wa kijinsia," katika timu yake ya makamishna 28.

Akianisha kuwa tangu kuanzishwa kwake mwaka 1958, chini ya asilimia 20 ya makamishna ndiyo wamekuwa wanawake, alisema: "Tunawakilisha nusu ya idadi ya watu wetu. Tunahitaji mgao wetu wa haki."